Maina (mpatanishi): Hamjambo Amina na Abdala. Ningependa kuwakaribsha kwenye kikao cha leo hiki kikao cha leo. Mwanzo kabisa ningependa kujitambulisha. Mimi ndiye mpatanishi mteule ama mediator na kwa jina ni Maina Migwe, lakini katika kikao cha leo mwaweza kuniita kwa jina langu moja, Maina. Katika hiki kikao kunakuwanga sio kama kortini, kwa hivyo wakati mnazungumziana mnaitana kwa jina moja ambalo unaweza penda kuitwa nalo. Ningependa kuwapatia fursa pia nanyi muweze kujitambulisha na pia kutujulisha ni jina gani ungependa litumiwe. Tutaanza na nani? Ni Amina ama ni wewe Musa? Musa: Nitakua wa kwanza. Maina (mpatanishi): Amina ni sawa Musa akiwa wa kwanza? Amina: Ni sawa. Musa: Mimi naitwa Musa Abdallah, na nikiitwa Musa pia niko sawa. Maina (mpatanishi): Sawa, asante sana. Basi fursa ni yako Amina. Amina: Mimi naitwa Amina Abdallah na nikiitwa amina niko sawa pia. Maina (mpatanishi): Asante. Basi ni hiki kikao cha leo na ninajua tayari mmeshajulishwa ya kwamba kesi yenyu imeshapigwa msasa pale kortini na ikapatikana ya kwamba ilikua sawa itatuliwe kwa njia ya upatanishi ama njia ya mediation. Ndiposa name nikateuliwa kuwasaidia kutatua jambo lenu. Upatanishi ama mediation tukianza tu, ni njia mbadala ambayo inatumiwa badala ya kuenda kortini ama mahali ambapo mnatumia mawakili dhidi ya wengine. Vile vile, kwa sababu ya hili janga la Corona, ndio sababu tukaweza kulifanya kupitia kwa mtandao. Kwa sababu mnajua mambo ambayo kidogo yanasambaza lile janga, ni ile mambo ya kukaribiana sana. Ndio maana tukaifanya kwa njia ya mtandao. Tukiendelea hivyo ningependa kujua kama mnaweza kunipata vizuri. Mnaniskia vizuri na mnaweza kuniona na kuona mwenzako? Musa: Kwa upande wangu nakuskia na nakuona vizuri. Maina (mpatanishi): Na vile vile unamwona Amina? Musa: Namwona. Maina (mpatanishi): Amina nawe? Amina: Nawaskia nyote na nawaona pia. Maina (mpatanishi): Asante. Kwa hivyo kidogo tu tuweze kujipanga namna tutaendelea. Kwa vile tunaifanya kupitia kwa njia ya mtandao, wakati mwingine kunakuanga na matatizo ya kimitambo. Kwa hivyo wakati kuna matatizo kidogo ya kimitambo na upate hauko katika kikao, unaweza kuitumia nambari yangu ya simu ambayo tayari nimeshawapa ili kuweza kuwasiliana nami na ili niweze kuwapa muda kutatua matatizo kisha uweze kurejea. Wakati ule ambao utakua hauko pamoja nasi, kikao kitakua kimetulia, akuna mazungumzo yatakua yanaendelea mpaka wakati ambao utaweza unarudi ndio tuweze kuendelea. Mnaelewa? Mwaweza kunielewa? Amina: Naam. Musa: Twakuelewa. Maina (mpatanishi): Kikao cha leo nimekipangia masaa mawili na nngependa kujua kama mtakuwepo kwa huo muda. Amina: Nitakuwepo. Musa: Tutakuwepo Maina (mpatanishi): Asante. Wakati tunaendelea ikiwa utahisi uchovu na ungependa kupewa nafasi kidogo ya kupumua unaweza kunieleza kisha nasi sote tutaweza kuchukua huo muda kunyosha misuli alafu kisha turejee na tuendelee. Hio ni sawa? Amina: Hio ni sawa. Musa: Naam iko sawa. Maina (mpatanishi): Asante. Tukianza hiki kikao ningependa kuwajulisha ya kwamba hiki ni kikao cha faraga. Mambo yale yote ambayo tutakua tunazungumza hapa hayafai kuenda nje ya hiki kikao, ni sisi tu wahusika ambao tunafaa kuwa tunayajua. Kwa hivyo, mambo haya ambayo twayazungumzia hapa hayafai kusambazwa kwa wengine. Lakini ikiwa ni lazima, pengine uzungumze na wadau wako kuhusu mambo ambayo yanaendelea, ni lazima uweze kuwajulisha kwamba haya ni mambo ya faraga na hawafai kuyasambaza kwa wengine. Je mnaelewa hayo? Musa: Naam twakuelewa. Amina: Naelewa. Maina (mpatanishi): Vile vile ingawa hiki kikao ni cha faraga, kama kuna maneno ambayo yataibuka, mabayo yataashiria uwezekano wa mtu kujiumiaza ama kuumiza wengine ama kuharibu mali ama mambo ya kudhulumu waokoto ama mambo ambayo ni kinyume cha sharia, basi ni jukumu langu kuwajulisha polisi ama ambao watahusika na mambo ya kuweka usalama ama kuangalia mambo kama hayo. Je, mnaelewa hilo? Amina: Naelewa. Musa: Naam twakuskia na twakuelewa. Amina: Basi ningependa mnidhibitishie ya kwamba mambo yale yote ambayo tutazungumza hapa hamtayasambaza kwa wengine. Je mnanihakikishia hilo? Musa: Naam. Amina: naam. Maina (mpatanishi): Amina pia, asante sana. Vile vile ningependa kuwajulisha ya kwamba hiki kikao cha upatanishi wahusika huja hapa kwa hiari yao wenyewe. Hakuna yeyote anafaa kushurutishwa kuja hapa. Je ningependa kujua mmekuja hapa kwa hiari yenyu nyinyi wenyewe ama mmeshurutishwa? Amina: Nimekuja kwa hiari yangu. Musa: Nami pia nimekuja kwa yangu. Hatujalazimishwa. Maina (mpatanishi): Asanti sana. Ningependa kuwajulisha kazi yangu katika hiki kikao ni kuwasaidia kuweza kuzungumaza moja kwa moja, kuweza kubadilishana namna ama suluhu ambazo mnafikiria tunaweza kuzitumia kutatua hili jambo ambalo tuko nalo. Vile vile kazi yangu ni kuweza kunakili ule mkataba ambao mmeweza kuupata kupitia kwa haya mazungumzo. Je mnaielewa kazi yangu katika hiki kikao? Amina: Naelewa. Musa: Naelewa. Maina (mpatanishi): Kuna swali lolote kuhusu kazi yangu kwenye hiki kikao? Amina: La. Maina (mpatanishi): Kazi yenu katika hiki kikao ni gani? Kazi yenyu ni kuzungumziana moja kwa moja mkizifwata sheria zile ambazo nitawajulisha hivi punde, kuwa wazi, kuwa tayari kumskiza mwenzako, kujaribu kutafuta suluhu, na kukubaliana namna ya kutatua tatizo lililo kati yenyu. Je mnaielewa kazi yenyu? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Kuna swal lolote kuhusu kazi yenyu? Amina: la. Musa: La. Maina (mpatanishi): Basi mwaweza kuwa na marafiki ama wale watu ambao huwa pengine mnazungumza nao wakati mko na mambo magumu, na kama mtaenda kuwaomba mawaidha, ama pengine mko na mawakili, hao watu kazi yao ni kuwapatia mawaidha na kuwapatia usaidizi wowote ule ambao mngehitaji wakati tunaendelea na hiki kikao. Je mmelewa kazi ya wengine bali na nyinyi na mimi? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Kuna swali lolote kuhusu kazi yao? Amina: la. Musa: Kwa sasa hatuna. Maina (mpatanishi): Basi kama hakuna, jambo lingine sasa ningependa kuwajulisha kuwa hiki kikao huwa na sharia ambazo sisi sote lazima tuzifwate. Nafikiria kwanza wakati mmoja wenyu anazungumza, basi yule mwingine hafai kumkatisha, anafaa kusubiri mpaka wakati ambao nitampa ruhusa na yeye pia aweze kuzungumza. Sharia nyingine ni kwamba lugha na ishara mtazitumia wakati wa mazungumzo katika hiki kikao, lazime iwe ni lugha ya heshima. Kwa hivyo, haifai kuwa na matusi ama na kejeli. Sheria nyingine ni kwamba wakati tunazungumza ama tunataka kutaja yule mwingine basi lazima tutumie jina lake. Jina ambalo tayari tumeshakubaliana ya kwamba tutayatumia hapa. Kwa mimi mtaniita Maina huyu naye tutamwita Amina na wewe tutakuita Musa, kando nayale mengine tumekua tukiyatumia. Sheria nyingine ni kwamba hufai kurekodi kipande chocho cha hiki kikao kwa njia yoyote ile. Kwa sababu hiki ni kikao cha faraja. Hizo sheria mmeziskia na mkazielewa? Amina: Naam nazielewa. Musa: Naam, mimi pia nimeziskia na nimezielewa. Maina (mpatanishi): Asante. Basi ningependa mnihakikishie ya kwamba mtazifwata na kuheshimu hizo sheria. Hamtazikikuka. Ningependa kupata hilo hakikisho kutoka kwenu. Amina: Naam nitazifwata sheria Musa: Mimi pia nitafwata sheria. Maina (mpatanishi): Asante sana. Jambo lingine ningependa kuwaelezea kidogo kwa ufupi ule mkondo ambao tutafwata katika hiki kikao, na hiki kikao huanza na mpatanishi wenu akiwapatia mazungumzo kidogo kidogo kuhusu mambo geni kuhusu hiki kikao. Hakuna lingine ambalo linafwata, ni nyinyi kupewa nafasi ya kupeana stori zenu. Ili muweze kunielezea ni mambo gani yaliyowaleta katika kikao. Mambo gani hayo ambayo mngependa kuyazungumzia na kuyasuluhisha. Kisha, wakati mnafanya hivyo nitakuwa kidogo nanakili maneno ambayo ninayasikia ili kuweza kutengeneza ajenda. Nikishatengeneza ajenda nitawasomea, nitawaonyesha na tukubaliane kwamba hayo ndiyo mambo ambayo mngependa kuzungumza, basi nitawapatia nafasi ya kuzungumza moja kwa moja na kutafta namna ya kusuluhisha hayo maneno, na vile vile wakati mwingine kutakua na kikao cha faraja ambapo nitakua naskiza kila mmoja wenu akiwa peke yake na yule mwingine pia nimpe nafasi katika kikao cha faraga. Nitawapatia muda sawa. Kwa hivyo kila mtu atapata muda sawa na yule mwingine, na baada ya hicho kikao tutarejea kwa kikao cha pamoja ambapo tutaendelea na mazungumzo na tutakubaliana namna ya kusuluhisha mzozo wenu. Basi kama nitaweza kupata suluhu, nitainakili, nitatia sahihi mwisho wa kikao. Je mnaelewa mkondo ambao mtafwata katika hiki kikao? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Kuna maswali yoyote? Amina: Kwa sasa hakuna. Maina (mpatanishi): Asante, basi kama hakuna kwa sasa tunaweza kuendelea nahuu ndio wakati wenu sasa wa kuweza kuelezea kile ambacho kiliwashinikiza kuenda kortini ama kuja katika hiki kikao cha upatanishi. Ni mambo gani hayo mngependa kusuluhisha? Ningewaliza kwa sasa, nani angependa kuwa wa kwanza kuelezea mambo yaliwaleta katika hiki kikao na ni mambo gani ungependa kusuluhisha? Musa: Naam, ningependa kuwa wa kwanza. Maina (mpatanishi): Sawa, Amina ni sawa Musa akianza? Amina: Naam ni sawa. Maina (mpatanishi): Basi Musa unaeza endelea, ueleze kile kilikuleta hapa, ni mambo gani muhimu ungependa kusuluhisha leo. Musa: Vile nimesema naitwa Musa Abdallah, mimi ndiye mtoto wa kwanza na mtoto wa kiume pekee wa marehemu Mama Halima. Mama Halima, mama yetu alifariki, lakini akamwachia dadangu Amina mali yake yote, akamwachia nyumba yake ambayo ni nyumba ya family, nyumba ambayo sote tuezaliwa hapo na tumelelewa hapo. Maina (mpatanishi): Kidogo tu ili niweze kuhakikisha nimekupata. Unasema ya kwamba mama yenyu aliaga,na wakati aliaga kuna nyumba ambayo alimwachia Amina. Musa: Ndio, nyumba ya family. Maina (mpatanishi): Nyumba ya familia. Alimwachia kwa njia ipi? Musa: Alimwachia kwa will yake. Alimwandikia yeye hio nyumba. Maina (mpatanishi): Kwa hivyo unasema kwenye will ya marehemu mama yenu alimwachia Amina nyumba? Haya endelea basi. Musa: Baada ya nyumba pia kulikua kuna pesa mama yetu tukawa nazo kwa benki. Hizo pesa ikawa kwa will yake pia amemwachia zote dadangu Amina. Maina (mpatanishi): Kwa hivyo unasema kulikua na pesa kwenye benki. Ni kiasi gani hiki cha pesa? Musa: Yafika karibu two millon, milioni mbili. Maina (mpatanishi): Milioni mbili? Musa: Naam Hizo pia alisema ameachiwa Amina. Alafu kuna gari ya Toyota, gari ya zamani, hilo ndilo pekeake mama ameniandikia mimi. Maina (mpatanishi): Kwa hivyo unasema kwamba kwa ile will kile ambacho umeweza kuachiwa wewe ni gari? Musa: Eeh pekeake. Maina (mpatanishi): Na hivyo vitu vininge vikaachiwa Amina? Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Kuna jambo lingine ambalo ungependa kuongezea? Musa: Kwa sasa ni hayo maneno ningependa kuzungumzia na kupata suluhu ambayo itatufurahisha sote wawili. Maina (mpatanishi): Wakati hii will inatengenezwa na Amina ikiwa zile vitu ambazo ameachiwa na wewe ukaachiwa zile vitu ambazo umeachiwa, hili jambo unalihisi namna gani? Musa: Mimi kusema kweli lilinifanya very sad na sina furaha. Mamangu nilikua nampenda, tulikaa pamoja kwa hiyo nyumba, nazaliwa hapo, nalelewa hapo, na vile hajaniandika kwa hiyo will ama alimwachia dadangu hiyo nyumba na pesa zake, ni kama kuwa wamenisahau ama amenitupa. Mimi nilikua sina furaha. Nimesikitika sana. Maina (mpatanishi): Kwa hivyo unasema hili jambo la mali kugawa kwa njia ambayo amegawa kwa ile will limekusononesha? Musa: Sana tena. Maina (mpatanishi): Je kuna jambo lingine lolote la ziada ungependa kuongeza? Musa: Kwa sasa sina la ziada. Ni haya ndiyo ya kuzungumza. Maina (mpatanishi): Asante sana Musa kwa kuweza kupeana story yako na Amina pia ningependa kukushukuru kwa kuskiliza bila ya kukatiza. Sasa ni wakati wako na wewe pia uweze kunipa story yako na kunielezea ni nini haswaa kilikuleta mwenyewe kwenye hiki kikao, na unaweza kunielezea ni nini bila kujibu yale Musa tayari ameyataja. Amina: Majina yangu ni Amina Abdallah, msichana wa pekee wa marehemu mama Halima, na kwa usia wake mama aliniachia nyumba na pesa zilizokua kwenye benki, kwa kua mama alipokua akiugua ni mimi nimemuuguza pale hospitalini, namtembelea kila siku namjulia hali na kumwangalia hadi alipofariki. Maina (mpatanishi): Kidogo tu ili niweze kuhakikisha nakupata vizuri, unasema ya kwamba mama alikua anaugua na wakati alikua anaugua pale hospitalini ulikua unamwangalia mpaka wakati amefariki. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Endelea. Amina: Kwa hayo mama akanieka kwenye usia wake amenipa nyumba na pesa pia na ningependa kuwa matakwa ya mama yafuatiliwe. Alivyotaka ndivyo yafanyike, kwa kuwa twafaa kumheshimu na alivyofikiria, fikra zake pia tuziheshimu kwa kuandika ule wosia wake. Maina (mpatanishi): Huu wosia unaozungumzia ni maneno gani yako kwenye huo wosia ambao unasema ungependa yafuatiliwe? Amina: Naam. Kwenye wosia mama ameniachia nyumba ya familia, tulipokua tangu kuzaliwa kwetu, pia ameniachia pesa zilizo kwenye benki, milioni mbili, na pia amemwachia ndugu yangu Musa gari la familia. Maina (mpatanishi): Kwa hivyo unasema kwenye wosia kuna nyumba, ambayo unasema wewe ndiye unafaa kuridhi, vile vile unasema kuna pesa kwenye benki. Hizi pesa unasema ni kiasi gani? Amina: Milioni mbili. Maina (mpatanishi): Na kuna milioni mbili kwenye benki ambazo pia ni wewe unafaa kuziridhi kulingana na huu wosia? Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Unasema kwamba kuna gari la familia ambalo linafaa kuridhiwa na Musa. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Una jambo la ziada? Amina: Kwa sasa sina. Maina (mpatanishi): Kulingana na mambo yalivyo, hili jambo ambalo mko nalo kati yako wewe na Musa, je linafanya uhisi namna gani? Amina: Nasikitika, ninahuzuni na pia ninahasira kwa kuwa huyu ni ndugu yangu ananipeleka korti kujaribu kutofautiana na yale matakwa ya mama, io pengine inaonyesha labda pengine amemkosea mama heshima na kuwa tumempoteza mama kwa hivyo tuna huzuni. Maina (mpatanishi): Nakuskia. Je kuna jambo lingine ungependa kutaja? Amina: Ningependa kupata suluhisho ili tuweze kuendelea na maisha. Maina (mpatanishi): Kwa hiyo ungependa mpate suluhu na hivi maisha yaendelee? Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Asante. Basi Amina ningependa kukushukuru kwa kunipa story yako, na ningependa kukushukuru wewe Musa kwa kukusikiliza bila ya kumkatiza. Musa: Ningependa kuuliza kitu. Maina (mpatanishi): Jambo gani? Musa: Dadangu alisema amekaa na mamangu hospitali ni ukweli na mimi pia nilikaa na mamangu hospitali. Yeye hakukaa na mama hospitali pekeyake. Hiyo ni kitu kama ndugu tumekua tukifanya kwa muda. Sasa kama yeye asema eti kaachiwa nyumba na pesa kwa sababu alikua akikaa na mama hospitali apo si... Maina (mpatanishi): Kidogo tu. Nitawapatia nafasi ya kuzungumzia hayo mambo kwa kirefu. Kwa sasa ningependa kwanza kuwaonyesha ile ajenda ambayo nimeweza kuinakili ili muweze kuona kama hayo ndiyo yale nimepata kwa mambo yale ambayo mngependa kuyazungumzia. Mnaweza kuiona ajenda ambayo nimeweza kuinakili? Ajenda ya kwanza ni nyumba. Je hayo mngependa kuyazungumzia na kusuluhisha? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Asante. Kuna jambo lolote pengine ambalo linaweza kuwa pengine sikuliskia? Ambalo sijaweza kulinakili ambalo mngependa tuongeze? Kuna jambo pengine nilikosa kuliskia? Ama ni hayo tu? Musa: Ni hayo tu. Maina (mpatanishi): Amina nawe? Amina: Ni hayo tu. Maina (mpatanishi): Asante basi kama ni hayo tu. Sasa basi ningependa kuwakaribisha ili muweze kuyazungumzia haya maneno moja kwa moja na ningependa kujua mngependa kuanza na jambo gani? Jambo la nyumba, pesa kwenye benki ama gari? Ni swala gani mngependa kuanza nalo? Musa: Mimi naona tungeanza na nyumba. Amina: Nakubaliana naye. Maina (mpatanishi): Amina unakubaliana naye? Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Okay. So ni nani angependa kulizungumzia kwanza? Na yule ambaye ataanza kulizungumzia ningependa umzungumzie mwenzako moja kwa moja nawe wakati unazungumziwa usikilize na uweze pia kupeana wazo lako ama fikra yako ama suluhu ambalo unafikiria unaweza kutumia kutatua jambo la nyumba. Nani angependa kuwa wa kwanza kuzungumza? Musa: Mimi ningefurahi kuwa wa kwanza. Maina (mpatanishi): Amina hiyo iko sawa na wewe? Amina: Naam ni sawa. Maina (mpatanishi): Basi Musa ningependa umweleze Amina kuhusu hili jambo la nyumba. Umuhimu wa hilo jambo kwako na namna zile ambazo mnaweza tumia kutatua hilo jambo la nyumba. Endelea Musa: Kama vile nimesema ile nyumba ni nyumba yetu ya familia sote wawili tumezaliwa hapo na tumelelewa hapo hapo nyumbani mpaka hivi tumekuwa watu wazima. Kwa wosia wake, ukweli mama amemwachia Amina hiyo nyumba lakini mimi naona hiyo itakua si sawa kwa sababu Amina kama msichana, yeye ni msichana ataolewa na atatoka pale kwa boma, na ile nyumba itabaki vile vile. Itakua hakuna mtu wa kukaa. Mimi kama mtoto wake wa kiume wa pekeake, mtoto wa mama wa kiume pekeake, mimi ndiye ninaona nina right kwa hiyo nyumba vile mimi nikaoa nimlete mke wangu hapo hapo, tukae kwa nyumba na ibaki hapo hapo kwa family. Haitatoka nje ama haitauzwa itabaki ndani ya familia yetu. Sasa kwa suluhu ambayo mimi naona... Maina (mpatanishi): Kidogo tu ili niweze kuhakikisha ya kwamba nimepata vile umesema. Umesema ya kwamba ungependa hiyo nyumba uridhi wewe, ukae pale ili vile vile ata baadae unaweza kukua na familia yako pale. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Amina ungependa kumjibu vipi Musa. Mwambie Musa fikra yako nawewe. Amina: Naam, ningependa kumwambia Musa kuwa naelewa anayosema. Maina (mpatanishi): Mwambie mojha kwa moja. Mzungumzie moja kwa moja. Amina: Musa naelewa unayosema. Lakini sioni ikiwa sawa kuwa wazo lako ni kuwa nitaolewa na nitatoka pale nyumbani lakini sioni hilo likiwa reason enough la kunifukuza kwenye nyumba ambalo umesema sote tulilelewa hapo, tulizaliwa pale. Musa: Sijakufukuza kwa nyumba. Nimesema tu mimi niridhi nyumba ibaki kwa family. Ama Maina nimemfukuza kwa maneno ambayo ninasema? Maina (mpatanishi): Niko hapa kuwasaidia kuzungumza moja kwa moja na kama kuna mahali ambapo unaona hajakuelewa unaeza muelezea kwa kirefu ili muweze kuelewana. Mnaweza kuendelea. Musa: Mimi ama Amina? Amina: Pengine Musa nilikosa kukuelewa. Nieleze tena. Musa: Mimi sijasema nataka kukufukuza kwa nyumba yetu ya family. Mimi nimesema mawazo yangu ni hii nyumba ibaki kwa jina langu kwa vile ibaki kwa family yetu. Ibaki in our family. Mimi nikioa mke wangu anaweza kuja pale, watoto wakawa pale pale. Wewe pia ukiolewa utatoka. Waeza kuregea nyumbani wajua una nyumbani, lakini wewe ukiolewa ukitoka ile nyumba nani atakaa pale? Kama wewe ndio occupant? Itakua nyumba itabidi iuzwe ama tuivunje, sasa kwa sababu twataka ile nyumba ibaki kwa family yetu, mimi naona itakua bora mimi ndio niwe na hiyo nyumba, kwa vile ibaki pale pale, na wewe wakaribishwa anytime kuja pale nyumbani, siwezi kukufukuza na ni nyumbani. Hivo ndio mimi nimemaanisha. Amina: Nakuelewa Musa kwa kuwa pia mimi nataka nyumba ibaki kwa familia lakini hata nitakapo olewa wajua nikitaka kutembea nyumbani nataka kuja na familia yangu tukae pia sisi pale tuenjoy nyumba ambayo mama ametuachia, kwa hivyo ninaona sitaweza kukaa na familia yangu na yako kwenye nyumba moja wakati mmoja kwa hivyo, sijui tutakavyofanya lakini na... Maina (mpatanishi): Amina una suluhu gani ambayo pengine ungeweza kumweleza Musa? Pengine mngeweza kujadiliana ama kuitumia. Una suluhu gani? Amina: Kwa sasa Musa anakaa kwa guest house ya nyumba yetu pale nyumbani. Pengine naweza kubali pengine aingie kwa nyumba kubwa nami nichukue ile nyumba ndogo ili aweze kukaa na familia yake in the future kwa ile nyumba kubwa na ninapozuru nyumbani nami niweze kuwa na mahali pa familia yangu kukaa. Maina (mpatanishi): Musa ungependa kumjibu vipi? Musa: Hilo ni suluhisho ambalo mimi pia nafurahi nalo. Mimi niko sawa kukaa kwa main house, guest house nitamwachia yeye akija yeye na familia yake watakaa pale bila ya kusumbuana. Maina (mpatanishi): Kidogo nikiwaskiliza, naskia ni kama kwamba mmekubaliana ya kwamba Musa aweze kuiridhi ile nyumba ya familia ama nyumba kubwa naye Amina aweze kuiridhi ile nyumba ya wageni ama guest house? Nimeweza kuwapata vizuri? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Basi hongera kwenu kwa kupata huo mkataba na sasa nafikiri tunaeza endelea kuzungumzia jambo lingine. Basi mngependa kujadilia ajenda gani? Bado kuna ile ajenda ya pesa kwenye benki na gari. Amina: Tungependa kuzungumzia pesa zilizo kwenye benki kwa sasa. Maina (mpatanishi): Kidogo sikuskia vizuri hapo. Amina: Nasema kuwa ningependa tuzungumzie pesa zilizo kwenye benki kwa sasa. Maina (mpatanishi): Na wewe Musa? Musa: Naam twaweza kuzungumza pesa ambazo ziko kwa benki. Maina (mpatanishi): Basi, Amina unaweza mwelezea Musa kuhusu fikra yako kuhusu zile pesa zko kwenye benki. Ungependa zifanywe vipi? Ni lipi ungependa mjadiliane na Musa ili muweze kusuluhisha hili jambo la pesa? Na wewe Musa utaweza kuskiliza na pia wewe kumpa Amina fikra zako. Musa: Sawa. Amina: Mama ameniachia milioni mbili zilizo kwenye akaunti yake kwenye benki na kwa hizo pesa twafaa kugharamia pesa zilizotumika hospitalini alipokua akiugua ambazo ni laki mbili na kwa hizo tutatumia laki mbili za hizo milioni mbili kulipia bill kwenye hospitali. Lakini baada ya hapo mama aliniachia zile pesa na naona kuwa itakua nikiziridhi pesa zile kwa kuwa tumekubaliana na Musa ya kuwa nitamwachia nyumba kubwa, niingie kwa nyumba ndogo, na pia alivyotueleza hapa leo kuwa kama msichana natarajiwa kuolewa pia nihame nyumbani niende nianzishe nyumba yangu, kwa hivyo, naona kuwa pesa zile nibaki nazo kwa kuwa nyumba ina kila kitu. Ina televisheni, ina sofa, ina vyombo, ina vitanda, ina kila kitu na mimi ninapo hama sitakua na kuanzisha nyumba yangu kwa kuwa kwa hayo niziridhi pesa zile ambazo mama ameniachia. Maina (mpatanishi): Kidogo tu. Musa ungeweza pengine kumwelezea Amina vile umeweza kuelewa maneno ambayo umeyataja? Musa: Nimemskia maneno ambayo amesema lakini si agree na yeye. Yeye amesema vitu viwili. Maina (mpatanishi): Amesema nini? Musa: Mwanzo tukianza hii mediation amesema yeye kwake kukaa na mama ndio maana amemwachia hivi vitu vyote. Hiyo mimi siagree nayeye. Mimi pia nilikaa na mamangu mpaka pale amekufa. Kama hilo ndilo sababu ya kuridhi basi mimi pia nina right ya kuridhi. Kwa sababu mimi pia nimekaa na mamangi si yeye pekeyake. Ya pili akasema yeye ataolewa na itabidi aende kuanza nyumba yake kwa sababu guest house haina TV, haina nini, lakini hilo namwambia yeye yuaolewa si kama yuaenda kuoa. Mimi bado sijaoa, sijakua na mke, mi pia kazi yangu haijakua kubwa sana. Bado mimi pia nina haja na hizo pesa ambazo mama yetu amewacha. Na yes kwa wosia... Maina (mpatanishi): Kidogo tu wakati mnaendelea kuzungumza mnaendelea vizuri na ningependa kuwapongeza kwa ile jitihada ambayo mnaonyesha, mnazungumza. Mnaendelea vizuri kabisa. Basi ningependa kuuliza Musa, kuna suluhu gani unafikiria ambayo unaeza zungumzia Amina kuhusu hili jambo la pesa ambazo ziko kwenye benki. Musa: Kwa hili jambo la pesa, mwanzo vile amesema, kuna hiyo jambo ya deni ya hospitali, tulipe. Tukishalipa, hizo pesa ambazo zitabaki naona itakua haki tukigawanya fifty percent, fifty percent. Nusu kwa nusu. Maina (mpatanishi): Amina na Musa wakati mnazungumzia kuhusu garama ya hospitali, natumai ni garama ambayo mama aliweza kuipata akiwa pale hospitalini. Ni garama ya kiasi gani? Musa: Ni laki mbili. Maina (mpatanishi): Ni hivyo Amina? Amina: Naam laki mbili Maina (mpatanishi): Musa kama nimekupata vizuri unasema ya kwamba mngeweza, kwa fikira yako unafikiria kwamba mngeweza kutumia zile pesa ambazo ziko kwenye benki kulipia hiyo garama na zile pesa ambazo zitasalia mgawane kwa usawa? Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Amina ungependa kusema vipi? Amina: Nimeyaskia ambayo ndugu yangu amesema lakini bado sikubaliani kuwa twafaa kugawana zile pesa kwa asilimia hamsini kwa hamsini kwa kuwa ata kama amejieleza kuwa ataoa itabidi pia ajianzishe, lakini haanzishi bila chochote, yaani ana kitu cha kuanzisha nacho, kwa hivyo naona zile pesa tugawane asilimia sitini kwa asilimia arubaini. Sitini kwangu, arubaini kwake. Maina (mpatanishi): Musa? Musa: Hapana, sipatanani na yeye. Kwangu naona arubaini itakua kidogo sana, kwa sababu yeye si kama hakuridhi ile guest house. Aliridhi guest house. Sasa mimi naona maybe tufanye forty five, fifty five. Maina (mpatanishi): Na wakati unasema forty five, fifty five. Forty five kwa nani, fifty five kwa nani? Musa: Forty five kwangu, na fifty five nitamwachia dadangu. Maina (mpatanishi): Amina unafikiria vipi kuhusu vile musa alivyosema? Amina: Hapo naeza kubaliana naye, kuwa niridhi asilimia hamsini na tano, naye aridhi asilimia arubaini na tano. Ya zile pesa ambazo zitasalia baada ya kulipa kugharamia bill ya hospitali. Maina (mpatanishi): Basi kama nimeweza kuwaskia vizuri nimeskia ni kama mmekubaliana ya kwamba zile pesa ambazo ziko wkenye benki ambazo ni milioni mbili ziweze kutumika kulipia gharama ya hospitali ya kiasi ya laki mbili, na zile pesa ambazo zitasalia ambazo baada ya kulipa gharama, mgawane asilimia hamsini na tano kwa Amina na asilimia arubuaini na tano kwake Musa. Je ni hivyo ambavyo mmeweza kukuabaliana? Amina: Naam. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Hayo ndiyo makubaliano yenu? Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Hongera kwa huo mkataba na naona sasa jambo ambalo limesalia kwenye ajenda ni swala la gari. Musa, ungependa kummwambia Amina namna gani kuhusu hilo swala la gari? Musa: Swala la gari ni kwa wasia wake mama ameniwachia mimi gari na hili gari ni gari ya nyumbani kila mtu ambaye ana haja huwa anaitumia. Sasa hapo akuna haja ya kupigania mimi naona tu Amina aiwache gari kwa jina langu. Maina (mpatanishi): Amina? Amina: Ni sawa naweza wacha lile gari kwa jina lake, lakini ningependa kuwa Musa unikubalie lile gari ninatumia ninapofanya biashara zangu hapa na pale na pia itakapofika wakati wangu wa kuhama, lile gari pia nitumie kusafirisha vitu vyangu. Maina (mpatanishi): Musa? Musa: Naam, hapo ninakusikia na ninakuelewa na hiyo iko sawa. Nitakuazima gari pale unataka kufanya bashara na pale unataka kuhama. Kama nilivyosema hili gari ni ya nyumbani inayotumika kwa haja za nyumbani. Hiyo sawa. Maina (mpatanishi): Pongezi, na kama nimewasikia vizuri, kuhusu swala la gari, tumekubaliana ya kwamba Musa aridhi hilo gari, naye Amina aweze kulitumia wakati wowote ule analihitaji kufanyia biashara zake. Je huo ndio mkataba ambao mmeweza kuafikiana? Musa: Naam. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Hongera kwa huo mkataba wenu. Naona ni kama mmemaliza mambo yote kwenye ajenda, na ningependa kuwapongeza sana. Mmefanya jitihada, mmefanya kazi kubwa na mmeifanya kwa njia iliyo safi. Kwa sasa basi ningependa kuwaonyesha mkataba wenu ili muweze kukubaliana kama uo ndio ule mkataba ambao mumeweza kuafikiana. Nafikiri mnaiona screen yangu? Musa: Kwa upande wangu bado. Amina: Bado pia. Maina (mpatanishi): Na je sasa mnaiona screen yangu? Maina (mpatanishi): Naam. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Huu basi ndio mkataba wenu, ambao mmeweza kuafikiana leo. Mnayaona majina yenu pale, na pia nambari ya kesi yenu, na nakala ya mkataba nitaisoma na imeanza ikisema ya kwamba, sisi tulio tia sahihi hapa chini, ambao ni nyinyi wahusika katika hili jambo, mumekubaliana ya kwamba mzozo wenu ifuatavyo. Ya kwanza, Musa aridhi nyumba ya familia naye Amina arithi nyumba ya wageni ama ukipenda, guest house. Je ni hivyo mmekubaliana kuhusu swala la nyumba? Amina: Naam ni hivyo. Musa: Naam. Maina (mpatanishi): Asante na hongera. Ya pili, swala la pesa. Pesa zilizo kwenye benki zitumiwe kulipa gharama ya hospitali ya marehemu ya kiasi cha laki mbili na masalio yagawe kwa mfumo ufwatao. Musa 45% na Amina 55%. Je hivyo ndivyo mmekubaliana kwenye swala la pesa? Musa: Naam. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Hongera. Ya mwisho, swala la gari, Musa arithi gari aina ya Toyota nambari sajili KAA 320Y. Musa na Amina pia wanakubaliana Amina aweze kuiazima gari na kuitumia kwa biashara zake. Je huo ndio mkataba wenu kwenye swala la gari? Musa: Naam ni hivyo. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Hongera kwa mkataba huo ambao mumeweza kuafikiana leo tarehe nane, mwezi wa tano mwaka wa elfu mbili ishirini na moja. Basi majina yenu yako pale, na kuna nafasi zenu za kutia sahihi, alafu nami nitatia sahihi na nawatumia huu mkataba ili muweze kutia sahihi alafu kisha mtaurejesha na utaweza kuwasilishwa kortini ili korti iweze kuchukua huo mkataba wenu kama kauli ya mwisho katika kesi yenu. Tukifika tamati ya hiki kikao, ningependa kuwapatia fursa mtaje jambo moja ama mawili. Musa: Mimi ningependa mwanzo kua... nimefurahi kuwa umetuleta pamoja mimi na dadangu Amina, ukatukalisha pamoja tukazungumza haya maneno baina sisi wawili na wewe. Kwa hilo asante wewe na Suluhu Mediation Center. Umetusave time na pesa za kuenda kortini na kufanya litigation ambayo ingetuchukua miaka. Kwa hilo nimefurahi mimi na dadangu tumeelewana kwa haya madogo na asante. Hilo ndilo langu. Maina (mpatanishi): Asante Musa. Nawe Amina? Amina: Nami pia ningependa kusema asanti kwa mpatanishi wetu, bwana Maina, kwa kuwa ndugu yangu nami tumekua pamoja kwa hivyo si vizuri tukiishi kama tuna hasira ama tukiishi bila kupatana, kwa hivyo Suluhu Mediation Center tunawapongeza sana kwa kutupanisha tena kutusave, kama Musa alivyosema muda mwingi na pia pesa zinazotumika pale kortini. Asanteni sana. Maina (mpatanishi): Asante, na hongera tena kwenyu wawili kwa kazi kubwa mlioifanya na kuweza kuafikiana na kupata huu mkataba, na vile vile nyinyi wenyewe mumejionea ya kwamba kupitia njia ya upatanishi, mizozo inaweza tatuliwa haraka na haina gharama kubwa. Na vile vile, kwa hii njia ya mtandao ama virtual mediation, naona ya kwamba pia hamjatumia nauli kutembea, hakuna uchovu, hakuna ile risk ya kupata magonjwa kama Corona. Kwa sasa mnaona watu hawatembei sana na mnaona mnaweza kupata suluhu kwa mambo yenu mkiwa pale pale nyumbani kwa gharama ya chini. Amina: Naam. Maina (mpatanishi): Mnaona akuna tofauti na kule kortini. Basi kutoka kwangu ni kuwashukuru kwa vile mumeweza kufwata sheria ambazo nimeweza kuzitaja hapo mbeleni na pia kuweza kupata ambayo mumeyapata leo. Asanteni sana na nawatakia kila la heri. Kwaherini kwa sasa. Amina: Asante. Kwaheri.